Uraibu

Updated 2/12/25 by Cindy Beall

Mistari ya Biblia
Mipango ya Biblia

Maombi

Baba Mungu, asante kwa kuwa hakuna jambo lolote tunaloshindana nalo lisilowezekana kwako kushinda. Wewe uko juu ya vitu vyote, na ndani Yako, vitu vyote vimeshikamana. Wasaidie ndugu na dada zetu watambue kwamba uraibu wao hauonyeshi utambulisho wao au thamani yao. Hao ni watoto Wako, wanaoitwa kwa jina lako, na kutengwa kwa makusudi Yako. Waonyeshe kwamba minyororo yao imekatika.

Wasaidie kupinga majaribu ili waweze kukumbatia utimilifu Wako wa maisha. Wape nguvu Zako za kupigana pale wanapohisi kulemewa, na waweke watu katika maisha yao ambao watawaunga mkono. Linda miili, mioyo na akili zao. Uwalinde na majaribu, na uwaokoe na uovu.

Katika jina la Yesu, Amina.


How did we do?

Powered by HelpDocs (opens in a new tab)